Yanga wakabidhiwa milioni zao

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Msemaji wa Serikali Gerson Msigwa leo amekabidhi kitita cha Tsh Milioni 10 kwa klabu ya Yanga baada ya kufunga mabao mawili katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United


Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe alipokea fedha hizo kwa niaba ya klabu katika Mkutano na Wanahabari uliofanyika Makao Makuu ya klabu ya Yanga Jangwani jijini Dar es salaam mapema leo


Fedha hizo ni bonus anayotoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan kwa kila bao linalofungwa na klabu za Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na kombe la Shirikisho barani Afrika


Yanga imekusanya jumla ya Tsh Milioni 50 kutoka mabao 10 waliyofunga kwenye michuano ya kombe la Shirikisho

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post