Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Leo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ilikutana kujadili maombi ya Feisal kwa Kamati hiyo akiomba mkataba wake na klabu ya Yanga uvunjwe
Simon aliiwakilisha Yanga kwenye shauri hilo ambalo hata hivyo halikusikilizwa baada ya upande wa Feisal kushindwa kutimiza baadhi ya matakwa ya kisheria. Shauri hilo limepangwa kusikilizwa tena May 04 mwaka huu
Akizungumza na Wanahabari muda mfupi baada ya kutoka kwenye Kikao cha Kamati, Simon alisema Yanga haina pingamizi kwa Feisal kuondoka anachopaswa kufanya ni kufuata utaratibu ambao unafahamika
"Nafikiri tulishaweka wazi msimamo wetu kupitia taarifa tuliyoitoa huko nyuma. Hatuna pingamizi lolote juu ya mahitaji ya Feisal"
"Anayemuhitaji Feisal aje klabuni au yeye akitaka kuondoka aje klabuni utaratibu anaujua tupeane mkono wa kwaheri," amesema Simon
Post a Comment