Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati homa ya mchezo wa Yanga dhidi ya Rivers ikizidi kupanda Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Kassim ameiunga mkono kampeni ya kununua tiketi za mchezo huo.
Waziri Majaliwa amenunua tiketi 500 za mchezo huo wa mkondo wa pili wa Robo Fainali kati ya Yanga dhidi ya Rivers ya Nigeria utakaopigwa Jumapili Aprili 30 Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Majaliwa anaungana na makundi mengine ya wadau 26 waliokuwa wameshanunua tiketi hizo za mzunguko ambapo tayari jumla ya tiketi 3540 zimeshanunuliwa.
Mbali na Majaliwa wengine ambao tayari wameshanunua tiketi hizo ni Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji (500), sambamba na wajumbe wa kamati ya Utendaji ya klabu hiyo Alex Ngai(100), Gerald Kihinga (100), Yanga Makaga (200).
Wengine ni Ibrahim Samuel (100), Brenden Kachenje (100), Armadillo enterprise (100), Crispo Hezron (100), Zahoro Matelephone (100), Jet &Sons (100), Bullet force security (100), Chicasa General traders (100), Tradeland commodities (100).
Wamo pia Anastacia Mbunda (100), Imtiaz Lalji (100),Tawi la Yanga Twitter Family (120), Feedlance intelligent feeding (100), Tawi la Mzumbe Alumni (200), Tosh Cargo Logistics (100), Nyambaya Cargo (100), Yanga whatsap Groups Admin (120).
Shirika la Bima la Zanzibar ZIC (100), Ramadhan Mlao (100), Tawi la Yanga Elite (500) na Tawi la Yanga Bungeni (100) na kufanya mpaka hapo Yanga kuuza tiketi jumla ya tiketi 3540 kwa ununuzi wa makundi hayo sawa na Sh 17,700,000 milioni.
Tayari klabu hiyo mapema jana walishatangaza kumalizika kwa tiketi za eneo la VPA za mchezo huo ambao endapo Yanga itakulinda ushindi wao wa awali ugenini waliposhinda kwa mabao 2-0 au kushinda tena au kutoa sare yoyote watatinga hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa mara ya kwanza katika historia ya klabu hiyo.
Chanzo: Mwanaspoti
Post a Comment