Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu za Tanzania Simba na Yanga zitakuwa kwenye majukumu ya kupeperusha bendera ya nchi mwishoni mwa wiki hii kwenye mechi hizo za robo fainali
Jumamosi April 22 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, saa 10 jioni Simba itawakabili mabingwa watetezi wa ligi ya mabingwa Wydad Athletic, VAR itatumika katika mchezo huu wa mkondo wa kwanza na pia itatumika katika mchezo wa mkondo wa pili utakaopigwa Morocco April 29
Jumapili April 23, Yanga itakuwa ugenini huko Nigeria kuikabili Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza kombe la Shirikisho, VAR pia itatumika
Mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30 ambapo teknolojia ya VAR pia itatumika
Post a Comment