Umri ni namba tu, Hawa hapa mastaa wa soka wenye umri mrefu

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Wanasema kazi na umri lakini kuna watu umri kwao sio jambo kubwa sana wao wameendelea kupiga kazi licha ya umri kuwa umeenda.


Moja kati ya maajabu ya hivi karibuni ni mchezaji wa kimataifa wa Japan Miura Kuzuyoshi kuweka rekodi yakuwa mchezaji mkubwa zaidi kufunga bao kwenye soka la ushindani akiwa na umri wa miaka 56.


Stori nyingi zimeandikwa kuhusu yeye, lakini hayupo peke yake kuna kundi kubwa la wachezaji ambao wameendelea kucheza soka la ushindani licha ya umri kuwatupa mkono.


1. Miura Kazuyoshi 56


Kwa sasa huyu ndio anashikilia rekodi yakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuendelea kucheza soka la kulipwa kwa sasa anaichezea Oliveirense inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Ureno (Liga Portugal 2), akiwa hapo kwa mkopo akitokea Yokohama FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Japan.


Amewahi kushiriki michuano mbali mbali ya kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Japan ambapo ameshiriki michuano ya AFC Asian Cup mwaka 1992 ambapo walikuwa mabingwa na 1996 AFC Asian Cup Kiujumla amecheza mechi 89 akiwa na timu hiyo ya taifa na kufunga mabao 55.


Jina lake la utani wanamuita "King Kazu" kwa upande wa klabu amecheza kwenye timu za nchi mbali mbali ikiwemo Brazil, Japan, Italy, Croatia, Australia, na sasa Ureno, akiwa ametumika wa misimu 38 hadi sasa.


2. Gianluigi Buffon 45


Sio jina geni, moja kati ya zawadi kubwa sana kuwahi kutokea nchini Italia, Buffon mwenye umri wa miaka 45 kwa sasa anaichezea Parma inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Italia.


Akiwa na Italia ameshiriki michuano mbali mbali mikubwa ikiwemo Kombe la Dunia mwaka 1998, 2002, 2006, 2010 na 201, pia akashiriki michuano ya Euro mwaka 2004, 2008, 2012 na 2016. Taji pekee alilofanikiwa kulipata akiwa na Italia ni kombe la Dunia mwaka 2006.


Kiujumla timu tatu tu kwenye maisha yake ya soka, na alicheza msimu mmoja tu nje ya Italia ambapo ilikuwa ni wakati anaichezea Paris Saint-Germain.


Buffon alianza kucheza soka la kulipwa mwaka 1995 akiwa na Parma kabla ya kujiunga na Juventus akiwa na timu hizo mbili amecheza mechi 520 za Seria A.


3. Endo Yasuhito 43


Mwamba mwingine kutoka Japan. Kwa sasa anaichezea Jubilo Iwata inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza nchini Japan.


Anacheza nafasi ya kiungo na akiwa na timu ya taifa ya Japan amecheza Kombe la Dunia mara tatu mwaka 2006, 2010 na 2014.


Kisha akacheza AFC Asian Cup mwaka 2004, 2007, 2011 na 2015. Amefanikia kuchukua mataji mawili tu akiwa na Japana ambayo ni yake ya AFC Asian Cup mwaka 2004 na 2011.


Katika maisha yake ya soka yote hajawahi kucheza nje ya Japan na alipata mafanikio makubwa akiwa na Gamba Osaka ambapo amecheza mechi 600 za ligi ndani ya miaka 20. amefunga mabao 15 akiwa na Japan.


4. Joaquin Sanchez 41 Winga huyu wa kimataifa wa Hispania kwa sasa anaichezea Real Betis akiwa na Hispania aliiwakilisha nchini hiyo mara mbili kwenye Kombe la Dunia mwaka 2002 na 2006 na Euro mwaka 2004. Akicheza jumla ya mechi 51 na kufunga mabao 4.


Joaquin anatajwa kuwa ni lejendi wa Real Betis akiwa na umri wa miaka 41, bado ameendelea kucheza kwenye soka la ushindani.


Katika maisha yake ya soka amecheza Valencia, Malaga, na Fiorentina, kwa sasa anashikilia rekodi yakuwa mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kufunga bao kwenye michuano ya UEFA Europa League.


5. Roque Santa Cruz 41


Bado anaendelea kuchachafya mastraika kwenye Ligi Kuu nchini Paraguay akiwa na Libertad. Straika huyu ana rekodi kibao kwenye soka la Paraguay akiwa amelichezea taifa hilo kwenye michuano mbali mbali ikiwemo Kombe la Dunia mwaka 2002, 2006 na 2010, Copa America mwaka 1999, 2007, 2011 na 2015. Akicheza jumla ya mechi 112 na kufunga mabao 32.


Mashabiki wa soka nchini Ujerumani na England watakuwa sio wageni wakilisikia jina lake kwani amecheza sana barani Ulaya akizitumikia Bayern Munich, Blackburn Rovers, na Manchester City akacheza pia Hispania na Mexico. Kwa sasa yeye ni ndio mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kwenye timu ya Libertad.


Chanzo: Mwanaspoti

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post