Ujumbe mzito wa Chama baada ya Simba kutolewa klabu bingwa CAF jana

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 Mara baada ya kuondoshwa kwa cha changamoto ya mikwaju ya penalti kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Kiungo Mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama, ameandika ujumbe mzito wa kuwashukuru mashabiki.


Simba walitolewa usiku wa kuamkia Aprili 29, 2023, kwenye Robo Fainali ya Pili iliyopigwa nchini Morocco na Wydad Casablanca kufanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 hivyo matokeo kuwa sare baada ya mchezo wa awali Simba nao kushinda 1-0.


Baada ya kuondoshwa kwa penalti, Chama ameweka picha ya kikosi cha Simba na kuandika ujumbe huu katika ukurasa wake rasmi wa Instagram:


Imekuwa ni safari ndefu yenye mambo mengi ndani yake na hisia mchanganyiko. Jana tulifanya kila kitu tunachokijua lakini mwisho wa siku ilibidi tukubaliane na ukweli ili tuweze kusonga mbele.


Shukrani za dhati kwa wachezaji, benchi la ufundi, Rais Mo, na mashabiki. Maombi na upendo wenu ndio umetufikisha hapa leo.


Tutachukulia matokeo ya jana kama chachu ya kuendelea kuimarika. Asanteni kwa ushauri na message zenu za kutia moyo. Mungu awabariki sana

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post