Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Klabu ya Juventus imepewa adhabu ya kucheza mchezo mmoja bila sehemu ya jukwaa moja la mashabiki wao baada ya kumtusi kwa kejeli za kibaguzi mshambuliaji wa Inter Milan, Romelu Lukaku
Lukaku alilengwa na mashabiki wa Juventus kabla na baada ya kufunga penati dakika ya tano ya muda ulioongezwa na kuwafanya Inter kutoka sare ya bao 1-1 katika mechi ya mkondo wa kwanza ya nusu fainali ya Coppa Italia iliyochezwa Jumanne iliyopita
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alipewa kadi ya pili ya njano kwa kuweka vidole kwenye midomo yake ili kuwanyamazisha mashabiki kwenye Uwanja wa Allianz
Bodi ya Ligi Kuu Italia, Serie A, imetangaza Juve lazima wafunge jukwaa moja la Kusini kwa mchezo wao ujao wa ligi ya nyumbani, ambao ni dhidi ya Napoli utakaochezwa Aprili 23, mwaka huu
Lukaku bado atatumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja katika mechi ya marudiano na Juve itakayochezwa Aprili 26, mwaka huu kwa kuonyeshwa kazi nyekundu.
Post a Comment