"Tunafahamu Simba wanarekodi hapa lakini kwa timu kubwa kama Wydad Casablanca hatuwezi kuhofia hili" Kocha mkuu wa Wydad

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Wakati Simba wakihakikisha wanafanya kila jambo kuibuka na ushindi dhidi ya Wydad jioni ya leo mchezo wa Robo Fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Sasa Kocha wa Mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Juan Carlos Garrido ameichimba Simba mkwara kuelekea mchezo huo.


Kocha huyo amesema washaisoma Simba vyema na kuwajua kiundani hivyo wanaingia katika mchezo huo wakiwa wanajua nini wanakwenda kufanya.


"Tunafahamu Simba wanarekodi hapa lakini kwa timu kubwa kama Wydad Casablanca hatuwezi kuhofia hili,tunahitaji kushinda popote tuendapo"


"Wydad kila msimu tunahitaji ubingwa wa ligi ya Mabingwa Afrika, hivyo utaona kwa timu kama hiyo inahitaji kushinda kila sehemu kama ambavyo tunahitaji kushinda hapa,"


"Jambo muhimu kwetu ni kufuzu hatua inayofuata’’tunajua ugumu wa mechi na tunafahamu mazingira tunayocheza,jambo muhimu ni kuzuia vizuri na kushambulia vizuri ili kupata matokeo,tunafahamu ubora na udhaifu wa Simna na tunajua kucheza ugenini si jambo dogo’"


"Kuhusu hali ya hewa ya mvua kwetu zio tatizo tumezoea kucheza na mvua hivyo tupo tayari kwa mapambano’"


Simba na Wydad wanakutana leo Jumamosi April 22 majira ya saa 10:00 katika Uwanja wa Benjamin mkapa Dar es Salaam.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post