Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Taarifa hiyo iliyotolewa na TP Mazembe imezima tetesi zilizokuwa zikimuhusisha Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi kutakiwa na Mabingwa hao wa Afrika mara tano
Kukosekana kwa Nabi kwenye benchi la ufundi katika mechi iliyopita dhidi ya TP Mazembe, kulitoa mwanya kuibuliwa kwa tetesi hizo ambazo zilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii
Nabi hakusafiri ya timu DR Congo akirejea kwao kufuatilia hati ya kusafiria
Nabi alisaini mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu kuendelea kuinoa Yanga
Wakati huu akikosekana, Kocha Msaidizi Cedric Kaze ameendelea kusimamia program za mazoezi pengine kesho atakiongoza kikosi cha Yanga katika mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold utakaopigwa uwanja wa Azam Complex
Post a Comment