Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Baada ya Yanga kuizamisha TP Mazembe kwenye dimba lao la nyumbani huko DR Congo kwa kuwachapa bao 1-0, US Monastir walipaswa kushinda angalau mabao matatu dhidi ya Real Bamako ili kuweza kuiondosha Yanga kileleni mwa kundi D
Monastir wakapata ushindi wa mabao 2-1 na hivyo kuihakikishia Yanga kumaliza kileleni mwa kundi D wakiwa na alama 13
Yanga sasa itakuwa na faida kwenye hatua ya robo fainali kwa kuanzia ugenini na kumalizia mechi ya pili nyumbani
Yanga, AS FAR, Malumo Galants na ASEC Mimosas zimemaliza vinara wa makundi wakati US Monastir, Rivers United, USM Alger na Pyramids zimemaliza katika nafasi ya pili
Katika hatua ya robo fainali Yanga itamenyana na kati ya Rivers United, USM Alger au Pyramids
Droo ya mechi za robo fainali itafanyika siku ya Jumatano
Post a Comment