Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Ni baada ya Singida Big Stars na Azam kushinda mechi zao za mzunguuko wa 25 na kujihakikishia nafasi za kuuungana na Yanga na Simba kukamilisha nafasi nne za juu
Vita iliyobaki ni kwenye nafasi ya ubingwa wa Ligi Kuu ambapo Yanga na Simba zinachuana huku pia kukiwa na vita ya nafasi ya tatu ambayo Singida BS na Azam Fc zinachuana
Pamoja na kujihakikishia ushiriki wa michuano ya CAF msimu ujao, lakini pia ni vita ya kuzoa Mamilioni ya Wadhamini wa haki za matangazo ya televisheni, Azam Media
Kwa mujibu wa viwango vya fedha ambazo klabu zinazoshika nafasi nne za juu kutoka Azam Media, Yanga hadi sasa kwa nafasi yake imejihakikishia Sh 500 Milioni, huku Simba ikiwa na uhakika wa Sh 250 Milioni
Singida BS kwa nafasi ya tatu imejiweka kwenye nafsi ya kuvuna Sh 225 Milioni na Azam ikifunga Nne Bora (Top 4) kwa Sh 200 milioni
Fedha inazopewa timu hizo zinazomaliza katika Nne Bora ni mbali na zile zinazotolewa na Mdhamini Mkuu wa ligi hiyo Benki ya NBC
Post a Comment