Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kuelekea mchezo dhidi ya Simba siku ya Jumapili, zilianza kuibuka tetesi kuwa klabu hiyo inamvizia beki wa kati wa Yanga Dickson Job ambaye kimsingi tayari alikuwa amefikia makubaliano ya kuongeza mkataba kuendelea kuwatumikia Wananchi
Imeelezwa Yanga imefunga mjadala na Job baada ya mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka miwili
Mkataba wake wa awali ulikuwa unamalizika mwishoni mwa msimu lakini sasa ni uhakika ataendelea kubaki na Yanga kwa miaka mingine miwili
Yanga imeendelea kuhuisha mikataba ya nyota wake ambao mwishoni mwa msimu watakuwa huru ili kuepuka mresha ya kusubiri mpaka mikataba yao ifikie tamati
Djigui Diarra, Yannick Bangala, Djuma Shabani, Mudathir Yahya, Bakari Nondo Mwamnyeto, Fiston Mayele, Farid Mussa, Zawadi Mauya ni miongoni mwa wachezaji ambao tayari mikataba yao imehuishwa
Post a Comment