Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumanne

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Graham Potter amekataa fursa ya kuchukua usukani kama meneja wa Leicester baada ya kutimuliwa Chelsea.(Talksport)


Potter atasubiri hadi msimu ujao kabla ya kuchukua kazi yake ijayo. (Mail) Meneja wa zamani wa Barcelona na Uhispania Luis Enrique ameibuka kama mtangulizi wa kuwa meneja mpya wa Chelsea. (Sun)


Chelsea wanataka kuwahoji mameneja watano kuhusu nafasi yao iliyo wazi, wakiwemo Enrique, Julian Nagelsmann, Mauricio Pochettino, Luciano Spalletti wa Napoli na mwingine mmoja. (Telegraph - subscription required)


Meneja wa Manchester United Erik ten Hag anaona nahodha wa Uingereza Harry Kane kama chaguo lake la kwanza la mshambuliaji msimu huu lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 yuko tayari kusajiliwa katika mkataba mpya Tottenham. (Athletic - subscription required)


Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim na bosi wa Eintracht Frankfurt Oliver Glasner pia wanazingatiwa. (Guardian)


Uongozi wa Chelsea una wasiwasi kuhusu umri wa mkufunzi wa zamani wa Bayern Munich Nagelsmann mwenye umri wa miaka 35. (Sky Sports)


Beki wa Uingereza Harry Maguire, 30, atauzwa United msimu huu huku Ten Hag akitoa wito kwa klabu hiyo kuwa na jeuri zaidi katika kukiondoa kikosini. (Manchester Evening News)


Manchester United wamefanya mazungumzo ya kiuchunguzi kuhusu kumsajili beki wa pembeni wa Ufaransa Benjamin Pavard, 27, kutoka Bayern Munich. (Athletic - subscription required)


United wameanza mazungumzo juu ya kumsajili beki wa pembeni wa Bayer Leverkusen na Uholanzi Jeremie Frimpong, 22. (Florian Plettenberg)


Tottenham watatafuta maoni ya Brendan Rodgers kuhusu kuwa meneja wao mpya kufuatia kutimuliwa kwake Leicester. (Football Insider)


Arsenal wamefanya mazungumzo na kiungo wa kati wa Ubelgiji Youri Tielemans, 25, ambaye mkataba wake na Leicester unakamilika msimu huu. (TeamTalk) Klabu ya Saudi Arabia ina nia kubwa ya kumnunua mshambuliaji wa Aston Villa na Brazil Philippe Coutinho, 30. (Football Insider)


Newcastle United ni mojawapo ya vilabu kadhaa vya Ligi ya Premia vinavyoonyesha nia ya kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City, Muingereza Taylor Harwood-Bellis, 21, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Burnley. (90min)


The Blues wameongeza nia yao ya kutaka kumnunua mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund, 20. (Mail)


Chelsea wana makubaliano ya mdomo kumsaini kiungo wa Ecuador Kendry Paez, 15, kutoka Independiente del Valle katika mkataba ambao unaweza kuwa na thamani ya zaidi ya £17.5m. (Standard)


BBC

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post