Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumatatu

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA

 
Rafael Benitez, Jesse Marsch, Ralph Hasenhuttl na Adi Hutter wote wanawania nafasi iliyo wazi ya meneja wa Leicester City. (mail)


Kufukuzwa kwa Graham Potter na Chelsea kutaibua shauku kubwa katika klabu ya Leicester City, huku meneja huyo akitajwa kuwa mrithi wa Brendan Rodgers. (Leicester Mercury)


Potter anaweza kupewa nafasi ya kurejea mara moja kwenye uongozi wa Leicester City. (Sport)


Mkufunzi wa Fulham Marco Silva anatajwa kuwa miongoni mwa wanaopewa nafasi kuwa meneja wa Chelsea. (Mirror)


Chelsea wanavutiwa na meneja wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann baada ya kumfukuza Potter, wakati kocha wa zamani wa Spurs Mauricio Pochettino pia ana mashabiki kwenye bodi. (Sport) Nagelsmann tayari amefuatwa kuhusu uwezekano wa kuwa meneja mpya wa Chelsea. (Fabrizio Romano)


Hata hivyo, Nagelsmann hana nia ya kumrithi Potter katika klabu ya Chelsea. (Sky Sports Germany via Mirror) Liverpool wamemtambua kiungo wa kati wa Chelsea na England Conor Gallagher, 23, kama shabaha kuu msimu huu. (Independent)


Arsenal wanawalenga wachezaji watatu katika safu ya kiungo msimu huu wa joto akiwemo Mchezaji wa Everton na Ubelgiji Amadou Onana, 21, Brighton na Ecuador Moises Caicedo, 21, na mchezaji West Ham na Uingereza Declan Rice, 24. (Football Insider)


Newcastle United wanapigiwa upatu kumsajili kiungo wa kati wa Leicester City na England James Maddison, 26. (Football Insider)


Chelsea wanajiandaa kuzuia nia ya Real Madrid kumnunua mlinzi wa Uingereza Reece James, 23, msimu huu na wanaweza kutoa kiasi cha pauni milioni 90. (Football Insider)


Aston Villa ni mahali pazuri zaidi kwa beki wa Southampton na Ghana Mohammed Salisu, 23, mwenye thamani ya £25m, kuliko Chelsea na Manchester United. (NipeSport)


Liverpool wanavutiwa sana na mchezaji wa Eintracht Frankfurt na kiungo wa kati wa Denmark Jesper Lindstrom, 23, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal. (Florian Plettenberg - Sky Sports Germany)


Vilabu vya Premier League vinamfuatilia kiungo wa Korea Kusini Lee Kang-in, 22, ambaye anatarajiwa kuondoka Mallorca msimu wa joto. (Fabrizio Romano)


BBC

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post