Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chelsea wanapanga kuuza nyota wake wengi kabla ya Juni 30 ili kusalia ndani ya sheria za kifedha - Financial Fair Play. (Evening Standard)
Mlinda mlango wa Manchester United Mhispania David de Gea, 32, yuko mbioni kusaini mkataba mpya wa kusalia katika klabu hiyo. (Forbes)
United wanaongoza katika mbio za kumsajili mshambuliaji wa Atalanta na Denmark Rasmus Hojlund mwenye umri wa miaka 20. (Mirror)
Barcelona wanakamilisha ofa ya kupeleka Paris St-Germain kwa ajili ya kumrejesha mshambuliaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 35 Lionel Messi. (Mundo Deportivo)
Aston Villa wameibua tena nia yao ya kumnunua kiungo mshambuliaji wa Arsenal na England Emile Smith Rowe, 22. (talkSPORT)
Villarreal wanatazamiwa kumpa beki wa Hispania Pau Torres kandarasi mpya huku Aston Villa wakipanga kujaribu kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 msimu huu. (Football Insider)
Manchester City wanataka kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Croatia Mateo Kovacic, 28, katika dirisha lijalo la msimu huu wa joto licha ya pia kutaka kusalia katika mbio za kumnunua nyota wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, 19. (Givemesport)
Paris St-Germain huenda wakamsajili kiungo wa kati wa Nice na Ufaransa Khephren Thuram, 22, au kiungo wa kati wa Lens na Ivory Coast Seko Fofana mwenye umri wa miaka 27 kama mbadala wa Bellingham. (CaughtOffside)
Newcastle wako tayari kumuuza winga Mfaransa mwenye umri wa miaka 26 Allan Saint-Maximin ili kupata fedha kwa ajili ya usajili katika dirisha lijalo la usajili. (talkSPORT)
Klabu za Manchester United, Newcastle, Wolves, Arsenal, West Ham na Crystal Palace zote zinamfuatilia beki wa pembeni wa Morocco na Bayern Munich Noussair Mazraoui, 25. (90min).
Beki Muingereza Chris Smalling, 33, yuko katika hatua ya mwisho ya mazungumzo na Roma ili kuongeza mkataba mpya kuendelea kusalia Italia hadi Juni 2025. (Fabrizio Romano).
BBC
Post a Comment