Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Chelsea wameamua kutomfuatilia kocha wa zamani wa Hispania Luis Enrique na badala yake wataelekeza nguvu zao kwa meneja wa zamani wa Paris St-Germain Mauricio Pochettino. (Telegraph)
Uamuzi wa The Blues wa kumkataa Enrique utafungua fursa kwa Tottenham kumpa mikoba Mhispania huyo, 52, kumrithi Antonio Conte. (Express)
Manchester United wana nia ya kumsajili beki wa kulia wa Uholanzi na Bayer Leverkusen Jeremie Frimpong, 22, huku United ikiwa tayari kuwatoa Muingereza Aaron Wan-Bissaka, 25, na Diogo Dalot wa Ureno, 24. (Mail)
Barcelona hawataweza kumsajili mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35, kutoka Paris St-Germain kutokana na hali zao ya sasa ya kifedha, anasema rais wa La Liga Javier Tebas. (Goal)
West Ham wamembainisha Paulo Fonseca wa Lille kama mbadala wa David Moyes, ambaye huenda akaachana na klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu (Guardian)
Arsenal wanaweza kumuuza mshambuliaji wa England wa Chini ya miaka 21 Folarin Balogun - anayecheza kwa mkopo katika klabu ya Reims ya Ufaransa msimu huu - kwenda RB Leipzig msimu wa joto ili kusaidia kufadhili uhamisho wa pauni milioni 100 kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice, 24. ( Metro)
Mshambuliaji wa Real Madrid na Ufaransa Karim Benzema, 35, ameongeza mkataba wa mwaka mmoja, na kumbakiza katika klabu hiyo ya Uhispania hadi 2024. (Mirror)
Winga wa AC Milan Mreno Rafael Leao, 23, amethibitisha kuwa anataka kusalia San Siro licha ya kuripotiwa kutakiwa na Manchester City. (Manchester Evening News)
Liverpool wako tayari kumsajili kiungo wa kati Adrien Rabiot ambaye atakuwa mchezaji huru, kandarasi ya kiungo huyo wa kati wa Ufaransa na Juventus ikitarajiwa kumalizika msimu huu wa joto. (Liverpool Echo)
Mshambuliaji wa Bayern Munich na Uholanzi Ryan Gravenberch, 20, ni mchezaji mwingine anayetazamwa na Liverpool wakati wanatafuta kurekebisha safu yao ya kati inayoyumba. (FourfourTwo)
Kiungo wa kati wa Ujerumani Toni Kroos, 33, anaweza kusaini mkataba mpya na Real Madrid licha ya ripoti kuwa huenda akastaafu. (Mail)
Tottenham wana nia ya kutaka kumnunua beki wa kati wa Chelsea, Levi Colwill, 20, ambaye amecheza kwa mkopo Brighton msimu huu. (Sun)
Chelsea wanaweza kumtoa mmoja ama wote wawili, kipa wa Senegal Edouard Mendy, 31, na Mhispania Kepa Arrizabalaga, 28, ili kumsajili kipa wa Borussia Dortmund na Uswizi Gregor Kobel, 25. (Bild)
BBC
Post a Comment