Tetesi za usajili barani ulaya Leo Jumatano

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane, 29, ndiye anayesakwa zaidi na Paris St-Germain msimu huu wa joto. (Le Parisien)


Meneja David Moyes kuna uwezekano mkubwa wa kuondoka West Ham msimu huu wa joto huku mchakato wa kubaini watakaomrithi ukiendelea. (Mail)


Jose Mourinho anaweza kuwa meneja mpya wa Paris St-Germain msimu ujao huku bosi huyo wa Roma akiwa kileleni mwa orodha ya mkurugenzi wa michezo wa PSG, Luis Campos. (RMC Sport)


Crystal Palace wanataka Roy Hodgson abaki katika klabu hiyo baada ya majira ya kiangazi ili kumshauri yeyote atakayechukua nafasi yake kama meneja ajaye wa Palace. (Telegraph)


Steven Gerrard anaripotiwa kuwa kwenye orodha ya wanaotajwa kusaka nafasi ya kocha mkuu ajaye wa klabu ya Olympiakos ya Ugiriki miezi sita baada ya kutimuliwa na Aston Villa. (Express)


Mazungumzo kati ya Alexis Mac Allister, 25 wa Brighton na Arsenal baso hayajafika popote. (Cesar Luis Merlo - via Twitter)


Barcelona inazidi kuamini kuwa mshambuliaji wa Argentina na Paris St-Germain Lionel Messi, 35, atajiunga tena na klabu hiyo msimu wa joto. (Sport)


United wanakaribia kukubaliana kandarasi mpya na mlinda mlango wa Uhispania David de Gea, 32, ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu huu. (ESPN)


Southampton wamemwambia kiungo James Ward-Prowse, 28, kwamba anaweza kuondoka msimu wa joto ikiwa klabu hiyo itashuka daraja. Tottenham, West Ham na Newcastle wote wanamtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England. (Sport)


Leeds itamsajili winga wa kimataifa wa Uhispania aliyechini ya miaka 19 Ilias Akhomach, 19, baada ya kushindwa kukubaliana na Barcelona kuhusu kuongezwa mkataba. (Sport)


Maskauti wawili wa Manchester United walimtazama winga wa akademi ya Birmingham City na timu ya taifa ya England ya Under-16 Trevan Sanusi, 15, siku ya Jumatatu. (Football Insider)


Beki wa kati wa Ivory Coast Eric Bailly, 29, atarejea United msimu huu wa joto huku Marseille wakikach kufanya mkataba wake wa mkopo kuwa wa kudumu. (Fabrizio Romano)


BBC

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post