Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Eriksen anarejea kwenye kikosi cha United kwa ajili ya mechi ya Jumamosi ya Ligi Kuu dhidi ya Everton kwenye Uwanja wa Old Trafford
Ten Hag ana furaha kiungo huyo wa Denmark amerejea kabla ya muda uliopangwa
Hata hivyo, bado amekasirishwa na jinsi jeraha hilo lilivyosababishwa na rafu kutoka kwa Andy Carroll
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Newcastle hakupewa kadi nyekundu kwa changamoto hiyo, ingawa baadaye alitolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano
"Haikuwa bure kwamba nilikuwa na hasira juu ya pambano hilo," alisema Ten Hag.
"Ilikuwa ni mchezo mbaya sana na jeraha baya. Nilidhani tulimpoteza kwa msimu mzima . Yuko mbele ya ratiba na tumefurahishwa sana na hilo," alisema
Ten Hag pia alithibitisha kuwa beki wa Uingereza Luke Shaw atakosa mchezo huo baada ya kuumia na kubadilishwa kipindi cha kwanza cha ushindi dhidi ya Brentford Jumatano
Ten Hag hakuthibitisha jeraha hilo lakini alisema ana uhakika Shaw atarejea hivi karibuni
Post a Comment