Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Wakati joto la mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Watani wa jadi Simba SC ambao watawaalika Yanga leo Jumapili katika uwanja wa Taifa jijini Dar ikiendelea kupamba moto mashabiki wa timu hizo kila mmoja ametamba timu yake kuibuka na ushindi.
Mchezo huo unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Soka Barani Afrika kuona nani ataibuka na ushindi baada ya tambo zao kudumu kwa muda mrefu tangu walipotoka sare ya kufungana goli 1-1 Oktoba 23 mwaka 2022.
Kingine ni nafasi ambazo timu hizo zipo Yanga ndio vinara kwa alama 68 huku Simba wakiwa nafasi ya pili kwa alama 60,utofauti wa alama Nane ambapo Yanga anahitaji kushinda ili kutangaza ubingwa huku Simba ikihitaji kuisimamisha na kurudi kwenye mbio za ubingwa.
Kufanya vizuri kwa washambuliaji wa timu hizo,Jean Baleke wa mwenye goli saba,Said Ntibazonkiza,Mosses Phiri wenye goli 10,John Bocco goli nane,Pape Sakho mwenye goli saba wote wa Simba huku kinara Fiston Mayele wa Yanga akiwa na goli 16 nao unachangia kwa kiasi kikubwa kila mmoja kutamani kuona katika mchezo wa leo watafanya nini.
Post a Comment