Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga inakabiliwa na mechi mbili za Ligi Kuu kabla ya kuwakabili Rivers United kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika utakaopigwa April 23 huko Nigeria
Keshokutwa Jumanne April 11 Yanga itaikaribisha Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Azam Complex
Jumapili April 16 mchezo wa pili dhidi ya Simba utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa. Hizi ni mechi mbili muhimu ambazo Yanga inahitaji kushinda ili kurahisisha mbio zake kuelekea ubingwa wa 29
Nabi alilazimika kusafiri Ubelgiji kuhuisha hati yake ya kusafiria akikosa safari ya Yanga DR Congo kuhitimisha hatua ya makundi ya Shirikisho dhidi ya TP Mazembe
Amekosa mechi mbili, mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold ukiwa wa pili Yanga ikitinga nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0
Post a Comment