Taarifa kamili kuhusu Hali ya Inonga na Aishi Manula

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Beki wa Simba SC Henock Inonga 'Baka' na golikipa namba moja wa klabu hiyo, Aishi Manula, wamefanyiwa vipimo na tayari wamerejea kambini kujiandaa na mchezo wa dabi ya Kariakoo utakaopigwa Jumapili Aprili 16, 2023.


Nyota hao walipata majeraha kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Ihefu FC na hawakuwa sehemu ya mchezo dhidi ya Ihefu wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa juzi Jumatatu Aprili 10, 2023.


Akizungumzia maendeleo yao, Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally alisema nyota hao pamoja na nyota wengine wote, wameingia kambini kujiandaa na mchezo huo wa dabi.


"Beki wetu Henock Inonga alipata kidonda kwenye mguu wake wa kulia, akatibiwa na leo anaungana na wenzake kambini. Aishi alipata majeraha ya bega akafanyiwa vipimo akanekana madhara aliyopata ni madogo hivyo akapewa mapumziko mafupi na leo anarejea kambini," alisema Ahmed.


Nyota hao pamoja na wengine waliokuwa majeruhi akiwemo Agustine Okrah, wote wamerudi kambini na jukumu litabaki kwa Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Roberto Oliviera 'Roberthinho' kuamua nani aanze kwenye mechi hiyo kubwa zaidi Afrika Mashariki na Kati.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post