Simba wakabidhiwa milioni 100 na Mbet

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kampuni ya M-Bet ambao ni Wadhamini wakuu wa klabu ya Simba, leo wamekabidhi hundi ya Tsh Milioni 100 ikiwa ni bonus baada ya Simba kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika


Ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kimkataba, M-Bet watatoa bonus kwa kila hatua ambayo Simba watavuka katika michuano hiyo


Mkurugenzi wa Masoko M-Bet, Allen Mushi amesema kitita hicho kilichokabidhiwa leo ni mwanzo tu, kuna fedha zaidi zitatolewa


"Mwaka jana wakati tunasaini mkataba moja ya kipengele ni kutoa bonus kwa kila hatua wanayofika kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kuanzia hatua ya makundi. Leo tunatoa Tsh. 100 milioni na tunawambia tu kuna zingine zitakuja," alisema Mushi


Nae Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula amesema wataendelea kuhakikisha Simba inakuwa klabu bora barani Afrika sasa ikiwa nafasi ya 7 kwa ubora


Kajula amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanja wa Benjamin Mkapa siku ya Jumamosi kuishangilia timu yao katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Athletic


"Mechi itachezwa siku yenye baraka, naomba kuwakaribisha Watanzania wote kuja kuangalia timu mbili bora zikicheza. Lengo letu ni kuwa klabu ya michezo bora barani Afrika. Tunaendelea kuboresha hilo kwa kuwa moja ya timu bora 10 Afrika na ndio timu pekee Tanzania ambayo itacheza CAF Super League"


"Tunawashukuru wadhamini wetu M-Bet kwa ushirikiano ambao wanatupatia," alisema Kajula

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post