Simba waja na mfumo mpya ukataji tiketi kuelekea dabi

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamesema kuelekea kwenye mchezo wao wa dabi dhidi ya Yanga SC, wameandaa mfumo mpya wa ununuaji wa tiketi ambao utawezesha kikundi cha wa watu kununua tiketi pamoja.


Akizungumza mapema hii leo Aprili 12, 2023, Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Imani Kajula, amesema wamekuja na mfumo huo ili kuleta ufanisi zaidi kwa mashabiki wa kikundi fulani kuweza kukata tiketi na kukaa eneo wanalotaka.


"Kuelekea mechi ya watani wa jadi, Simba inatangaza aina mpya ya tiketi ambayo ni Mnyama Ticket ambayo itawezesha marafiki ambao wanapenda kwenda pamoja uwanjani wanaweza kununua tiketi kama kundi."


"Hatupendi mashabiki wetu ambao wana kundi kupata shinda ya tiketi. Namba zitapatikana kwenye ofisi za Simba. Tunawaondolea changamoto ya kupanga foleni. Tunaamini siku ya Jumapili uwanja utajaa rangi nyekundu na nyeupe. Bei zinategemea na eneo," alisema C.E.O Imani Kajula.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post