Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Akiwa na kumbukumbu ya ushindi katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi, mshambuliaji Mkongomani, Fiston Mayele, amewahakikishia furaha mashabiki wa timu hiyo kwa sababu amejiandaa 'kutetema' ili atimize ndoto za kuifungia Yanga mabao akiwa kwenye ardhi ya nyumbani kwao
TP Mazembe itaikaribisha Yanga katika mechi ya kukamilisha ratiba ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayochezwa kesho mjini Lubumbashi, DRC.
Mayele, amesema licha ya Congo ni nyumbani kwao, lakini kazi iliyompeleka ni moja ambayo ni kuitumikia Yanga na kufikia malengo ya kuvuna alama tatu muhimu.
Mayele amesema wanahitaji kupata ushindi katika mechi hiyo na kuonyesha ubora wa kikosi chao pamoja na kumfurahisha mdhamini wao Gharib Said (GSM) ambaye ameambatana na timu huko Lubumbashi.
"Bosi wangu amekuja katika ardhi ya nyumbani kwangu, anahitaji kupata furaha katika mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe, timu kubwa kwa hapa Congo lakini Yanga ni kubwa Tanzania, malengo yetu ni kusaka pointi tatu muhimu katika mchezo wetu wa Jumapili"
"Sasa tunataka kushinda mechi hii ili kuonyesha ukubwa wa Yanga katika michuano ya kimataifa, nimewaahidi mashabiki kutetema katika uwanja uliopo nyumbani kwangu" alisema mshambuliaji huyo mwenye mabao matatu katika hatua ya makundi
Aliongeza benchi la ufundi limefanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza katika mechi iliyopita na sasa kazi kubwa imebaki kwa wachezaji kupambana kutafuta matokeo chanya ili kumaliza wakiwa kinara kwenye kundi lao
Post a Comment