Sadio Mane azichapa na Leroy Sane

Kupata Kifurushi cha bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


Nyota wawili wa FC Bayern Munich, Sadio Mané na Leroy Sané wamezua gumzo baada ya kuzichapa juzi muda mfupi baada ya mchezo wa UEFA Champions League dhidi ya Man City kwenye chumba cha kubadilishia nguo.

Picha zilizonaswa uwanjani ziliwaonyesha mastaa hao dakika ya 83 ya mchezo wakirushiana maneno baada kutofautiana wakati wakijenga shambulizi kwa Man City.

BILD Wameripoti kuwa Mané alilalamika kwa Sané kuhusu moja ya tukio uwanjani na kisha ghafla akampiga mdomoni Sane na kumwachia alama.

Wachezaji hao walitenganishwa na wenzao na Sané akatolewa nje ya chumba ili kutuliza ugomvi huku Mane akiondolewa kwenye chumba hicho cha kubadilishia nguo.

Hadi sasa, Bayern hawajazungumzia tukio hilo wala madhara yaliyotokea.

Bayern itakuwa na kibarua kingine kupindua meza kwa Man City kwenye mchezo wao wa marudiano katika Dimba lao la Allianz Arena jijini Munich baada ya kupoteza mchezo wa kwanza kwa bao 3-0.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post