Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba itavaana na Wydad kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika Afrika, hatua ya robo fainali Jumamosi April 22 ikiwa ni wiki moja tangu walipowachapa watani wao wa jadi Yanga mabao 2-0 kwenye Ligi Kuu Bara
Robertinho amesema malengo ya kikosi chake ni kuibuka na ushindi katika mchezo huo
"Kila mmoja wetu anatambua tuna mechi ngumu zinazokuja mbele yetu, hivyo tunahitaji kuhakikisha tunacheza kwa kasi ile ile kwenye kila mchezo, sasa ili kufanikisha hilo ni lazima tujiandae vizuri kimwili na kiakili"
"Tunafahamu, tunatakiwa kumaliza mchezo hapa Dar na kwenda ugenini tukiwa na kitu mkononi," alisema Robertinho
"Tunatambua malengo yetu kama klabu na sisi kama benchi la ufundi tunaandaa vizuri timu kwa ajili ya michezo ijayo, hatuna kisingizio kwa sababu huu ni wakati wa kuonyesha uwezo wetu kwa wapinzani waliokuwa mbeleni ambao tunafahamu ubora wao"
"Kucheza na Raja Casablanca, Horoya, Vipers ni dhahiri kuna kitu kikubwa wachezaji wanapata lakini hata sisi benchi la ufundi kwa maana ya kukutana na mbinu tofauti ambazo zinatuongezea ufanisi kwenye kazi," alisema
Wydad ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii wamechukua taji la CAF mara tatu kuanzia mwaka 1992, 1995 na 2022 na ilimaliza ya pili katika miaka ya 2011 na 2019 huku mara ya kwanza kukutana na Simba ilishinda 3-0 mwaka 2011
Katika kundi A, Wydad ilimaliza kinara na pointi 13 ikipoteza mechi moja tu ikicheza ugenini dhidi ya JS Kabylie ya Algeria, ikishinda nne na kutoka sare moja huku kwa upande wa Simba ikimaliza ya pili kundi C na pointi tisa
Kinara wa mabao Simba ni Clatous Chama mwenye manne wakati kwa Wydad ni mshambuliaji raia wa Senegal, Bouly Sambou mwenye mabao matatu pia
Mwanaspoti
Post a Comment