Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabao mawili ya Rodrygo yalitosha kuwaadhibu The Blues kwa kichapo cha 2-0 Stamford Bridge huku yakiwashuhudia Real Madrid wakitinga nusu fainali katika michuano ambayo imekuwa kawaida yao kushinda wanapofika hatua hiyo
Kikosi cha Frank Lampard kilihitaji kupindua kipigo cha mabao mawili kutoka kwa mechi ya kwanza ili kuwa na matumaini lakini haikuwezekana
Ilikuwa mechi ya nne mfululizo Lampard anapoteza tangu akabidhiwe mikoba ya kuwa kocha wa muda
AC Milan nao wakawaduwaza mabingwa watarajiwa wa Serie A Napoli kwa kuwalazimisha sare ya bao 1-1 katika uwanja wao wa nyumbani
Milan wametinga nusu fainali kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 kufuatia ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa San Siro
Mechi nyingine mbili za robo fainali zitapigwa leo, Bayern Munich wakiwa nyumbani watakuwa na kazi ya kupindua matokeo ya kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Manchester City wakati Inter Milan watahitaji kulinda ushindi wa mabao 2-0 waliopata ugenini dhidi ya Benfica
Post a Comment