Rais Samia awapongeza Simba Kwa ushindi

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dk Samia Suluhu Hassan ameipongeza klabu ya Simba kwa kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga katika mchezo wa ligi kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jana


Katika ujumbe wake alioweka kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Dk Samia amesema mchezo baina ya timu hizo watani unawakutanisha Watanzania wengi na kwa wakati mmoja na kuwapa burudani kwa namna ya kipekee


"Hongereni Simba kwa ushindi mliopata dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC. Upinzani wenu wa jadi uwanjani ni burudani inayowaleta pamoja mamilioni ya Watanzania kutoka katika kila kona ya nchi yetu, kwa namna ya kipekee," aliandika Dk Samia


Mabao ya Hennock Inonga na Kibu Denis ndio yaliyopeleka kilio Jangwani na kuwaacha watani wakiwa wamepigwa na butwaa baada ya kupelekewa pumzi ya moto kutoka kwa vijana wa Msimbazi!

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post