Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kikosi cha Simba kiko nchini Morocco kuelekea mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad ambao utapigwa Ijumaa, April 28 saa nne usiku
Akiwa miongoni mwa msafara wa pili wa viongozi ulioondoka Dar jana jioni kuelekea Morocco, Ahmed alisema wanakwenda Morocco kuandika historia ya kufuzu nusu fainali ya ligi ya mabingwa
Ahmed amesema Simba ina malengo makubwa kwenye michuano hiyo, Wydad watarajie kukumbana na wakati mgumu hapo hapo kwenye uwanja wao
"Tunawaheshimu Wydad, ni timu kubwa na mabingwa watetezi wa michuano hii lakini tunawaambia hatuwaogopi, tunakwenda Morocco tukiwa na malengo ya kufuzu nusu fainali"
"Nimesikia wameuza tiketi zote za mchezo, mimi nasema sisi tumefurahi kwani tunakwenda kuwaadhibu mbele ya mashabiki wao. Waombolezaji hata walie vipi kwenye msiba hawawezi kuamsha maiti," alitamba Ahmed
Simba itahitaji ushindi au hata matokeo ya sare siku ya Ijumaa ili kujihakikishia tiketi ya kucheza nusu fainali
Ikitokea imepoteza isiwe zaidi ya tofauti ya bao moja na iwapo Simba itafunga bao ugenini basi itatinga nusu fainali
Post a Comment