Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mwenyekiti wa timu ya Namungo,Hassan Zidadu amesema msimu huu haukuwa mzuri kwao lakini ushiriki wao kimataifa umechangia wao kukamiwa
Namungo inashika nafasi ya sita kwenye msimamao wa Ligi Kuu Bara, ikiwa na pointi 35,imecheza michezo 26 huku Yanga ikiongoza ikiwa na pointi 68 ikifuatiwa na Simba yenye alama 63
Timu hiyo ilishiriki Kombe la Shirikisho msimu wa 2020/21 na kushika nafasi ya mwisho kwenye kundi D lililokuwa na Raja Casablanca, Pyramids na Nkana
Zidadu ambaye ni Mbunge wa Tunduru Kaskazini alisema msimu huu wameshindwa kufanya vizuri lakini watakaa chini na kuja na mipango ya kuhakikisha wanafanya vizuri msimu ujao
"Tulijisahau kutoka na ule ushiriki wetu wa mashindano ya Kimataifa timu zimetuchukulia kama sisi ni wakubwa, lakini sisi wenye tunajiona wakawaida, hapo ndipo tulipoteleza wenzetu wanajitoa kwamba sisi ni timu kubwa lakini vijana wetu hawalielewi hilo"
"Kwetu sisi tunachukulia kama ni somo kwahiyo msimu ujao tutaenda kukaa chini ili kuelekezana kwamba kila mechi kwetu iwe kama fainali,"alisema Mwenyekiti huyo.
Zidadu aliwataka mashabiki wa Namungo kutokuwa na wasiwasi wanaweka mikakati ya kuhakikisha msimu ujao wanacheza mashindano ya kimataifa.
"Mafanikio ambayo tumeyaona katika ligi yetu ni udhamini sasa hivi timu zinaweza kusafiri na kulipa mishahara kwa wakati hili ni jambo kubwa sana"
Mwanaspoti
Post a Comment