Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kauli hiyo ya Nabi imekuja baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United, ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 2-0, katika Dimba la Godswill Akpabio, mabao yote yakifungwa na Fiston Mayele
"Sisi hatujaja hapa kujifurahisha, nazifahamu timu za Nigeria, kupata matokeo Nigeria ni vigumu sana, lakini tupo serious na mashindano haya. Siku zote nimekuwa nikiwaambia wachezaji wangu wajitahidi kupata matokeo mazuri ugenini kabla ya kuwaza matokeo ya uwanja wa nyumbani, ndicho hicho nilichokifanya"
"Rivers ni timu nzuri, mashindano ya Klabu Bingwa mwaka 2021/22, Rivers walituondoa katika hatua za awali, kulikuwa na sababu nyingi lakini zaidi timu yetu haikuwa kwenye ubora tulionao sasa hivi"
"Sisi Waafrika tunajuana, mechi hii haijaisha, bado kuna mechi nyingine ya marudiano Tanzania baada ya siku saba, kikao changu cha kwanza na wachezaji wangu itakuwa ni kuwasisitiza hilo. Nawaheshimu Rivers, kocha na wachezaji wao wote ni wazuri, lakini sisi tuna malengo ya kufika mbali zaidi kwenye mashindano haya," alisema Nabi
Post a Comment