Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Nabi aliwasili nchini jana mchana akitokea Tunisia kushughulikia masuala ya kifamilia
Nabi amesema kuna kazi kubwa iko mbele yao katika mechi zinazofuata na amewapa maelekezo wachezaji wake kuhakikisha wanaongeza bidii ili kufanikisha malengo yao
"Tuna ratiba ngumu mbele ikiwa ni pamoja na mechi ambazo zinaweza kuamua hatma yetu ya ubingwa wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa ya CAF. Nimezungumza na wachezaji ni lazima waongeze bidii ili tuweze kutimiza malengo yetu," Nabi aliiambia Yanga Media
Nabi amerejea wakati mwafaka wakati kikosi chake kikikabiliwa na mechi muhimu za ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar na Simba
Jumanne April 11 Yanga itacheza na Kagera Sugar uwanja wa Azam Complex kisha kufuatiwa na mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumapili, April 16 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Yanga itakuwa katika nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa kama itashinda mechi hizo
Mchezo wa kwanza wa robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Rivers United utapigwa April 23 nchini Nigeria na marudiano kupigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30
Post a Comment