Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Msemaji wa Klabu ya Azam, Zakaria Thabit 'Zaka Za Kazi' amemchana Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally baada ya kudai kuwa klabu hiyo haipendi mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika na haina mpango nayo.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii, #ZakazaKazi amesema;
Arsene Wenger, kocha wa zamani wa Arsenal, aliwahi kusema, When you give success to stupid people, it makes them more stupid
Unapowapa mafanikio watu wapuuzi, huwafanya wawe wapuuzi zaidi. Bwana mdogo @ahmedally_ anathibitisha kauli hii ya gwiji Wenger.
Mafanikio ya kufika robo fainali hizi mbili tatu yamemfanya awe mtu wa ajabu sana kiasi cha kutoa kauli zenye aibu kwa mpira.
Anasema hawana mpango na Kombe la Shirikisho kwa sababu ni dogo na zinashiriki timu mpya mpya.
Hebu tuanze kuangalia timu zilizofika robo fainali tangu msimu wa 2018/19 ambao Simba walianza kufika robo fainali za CAF
2018/19
Zamalek (1911)
RS Berkane (1938)
Étoile du Sahel (1925)
CS Sfaxien (1928)
Nkana FC (1932)
Al-Hilal (1930)
Hassania d'Agadir (1946)
Gor Mahia (1968)
2019/20
Pyramids (2008)
RS Berkane (1938)
Horoya (1975)
Hassania d'Agadir (1946)
Zanaco FC (1978)
Al-Nasr Benghazi(1954)
Al Masry (1920)
Enyimba (1976)
2020/21
JS Kabylie (1976)
Coton Sport (1986)
Raja (1949)
Pyramids (2008)
ASC Jaraaf (1933)
Orlando Pirates (1937)
Enyimba (1976)
CS Sfaxien (1928)
2021/22 - msimu wa moto
RS Berkane (1938)
Orlando Pirates (1937) - jeshi la zima moto
TP Mazembe (1939)
Al Ahli Tripoli (1950)
Simba S.C.(1936) wawasha moto
Al Masry (1920)
Pyramids (2008)
Al-Ittihad Tripoli (1944)
2022/23
Yanga (1935)
Asec (1935)
Rivers United (2016)
USM Alger (1937)
AS FAR (1958)
US Monastir (1923)
Marumo Gallants (2021)
Pyramids (2008)
Katika misimu hiyo mitano, jumla ya timu 32 zilifika robo fainali mara moja huku 8 zikijirudia zaidi ya mara moja.
Zenye umri mdogo zaidi ni tatu tu, Pyramids (2008), Marumo Gallants (2021) na Rivers United (2016).
Timu 10 zimeizidi umri Simba, zilizobaki zimepishana kidogo tu na timu ya Ahmed, lakini zina mafanikio makubwa zaidi Afrika.
Timu kama Coton Sport ya Cameroon, ilianzishwa 1986 lakini imeshafika hadi fainali ya ligi ya mabingwa...timu ya Ahmed haijawahi...inaishiaga robo tu.
Enyimba na Mazembe ndiyo usiseme...mbingu na ardhi kulinganisha na timu ya Ahmed.
Jeuri ya kusema Kombe la Shirikisho lina timu mpta anaitoa kwenye kauli ya Arsene Wenger...
Wale Makhirikhiri Jwaneng Galaxy waliovuaga jezi kwa Mkapa, walianzishwa 2014.
Post a Comment