Mexime azitaka pointi 3 za yanga

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime anaipigia hesabu kali Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Aprili 11 kuhakikisha anaibuka na alama tatu


Kagera Sugar ipo nafasi ya saba ya msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 32 ambapo inatarajia kuvaana na Yanga Aprili 11 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Mexime amesema kuwa, kikosi chake kipo vyema hivyo anajipanga kuikabili Yanga Aprili 11 ili kuweza kutwaa pointi tatu.


"Mchezo wetu unaofuata tunacheza na Yanga, siku zimeshakwisha hakuna muda wa kupumzika, tunahitaji kujiandaa ili kuweza kufanikiwa kutwaa alama tatu"


"Ligi ni ngumu na ina ushindani mkubwa hasa mechi hizi za mwisho kila timu inapambana kupata matokeo hivyo tunajipanga kuweza kupata matokeo mazuri," alisema Mexime


Mexime alimalizia kwa kusema kuwa, kikosi chake kipo vizuri hivyo wanajipanga kumaliza vizuri.


Ligi Kuu Bara ipo ukingoni ambapo kila timu imebakiza michezo mitano ili kukamilisha msimu wa 2022/23.

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post