Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mtanange huu utapigwa Jumapili, April 23 huko Nigeria katika uwanja wa Godswill Akpabio uliopo mji wa Uyo
Rivers United walitumia uwanja huo kwenye hatua ya makundi na baadae wakaomba kuruhusiwa kurejea kwenye uwanja wao wa Adokiye Amiesimaka huko Port Harcort ila Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limegomea mabadiliko hayo baada ya kufanyia ukaguzi uwanja huo na kubaini bado haukidhi vigezo
Yanga itakwenda Nigeria ikiwa na lengo moja, kusaka ushindi ugenini na hata ikishindikana kupata matokeo ya sare
Mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, April 30 2023
Malengo ya Yanga ni kufuzu nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga inaweza kufunga msimu huu ikiwa na mataji manne
Iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya NBC kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Simba inayoshika nafasi ya pili zikiwa zimesalia mechi nne tu, pia iko hatua ya nusu fainali kombe la Shirikisho la Azam, na inasaka nafasi ya kutinga nusu fainali ya kombe la CAF la Shirikisho
Mwanzoni mwa msimu ilitwaa Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba
Post a Comment