Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Stephane Aziz Ki alikuwa shujaa wa Yanga katika mchezo huo akifunga mabao matatu 'hat-trik', mawili yakiwa mikwaju ya penati na moja likiwa bao la 'kideo' akiwa umbali takribani mita 25
Dhamira ya ushindi kwa Yanga ilionekana mapema kwenye kipindi cha kwanza, Fiston Mayele alikuwa na uchu wa kuongeza mabao yake
Alifanikiwa kufunga bao kwenye kipindi cha pili baada ya kosakosa nyingi katika kipindi cha kwanza
Bernard Morrison nae amerejea na bao lake, akiweka kambani bao la nne kwa shuti kali akiwa nje kidogo ya 18
Ilikuwa mechi ambayo Yanga walitawala na pengine walistahili kufunga zaidi ya mabao matano
Mayele amejiimarisha kileleni katika mbio za ufungaji bora akifikisha mabao 16, idadi sawa ya mabao ambayo alifunga msimu uliopita
Mabao yake matatu aliyofunga Aziz Ki leo, yamemfanya afikishe mabao nane msimu huu wakati Morrison amefunga bao lake la tatu leo
Yanga imerejesha gap la pointi nane dhidi ya watani zao Simba baada ya kufikisha alama 68 kileleni mwa msimamo wa ligi
Ushindi katika mchezo unaofuata dhidi ya Simba, utaihakikishia Yanga ubingwa kwani kimahesabu watahitaji alama mbili kutoka mechi nne zitakazokuwa zimesalia
Post a Comment