Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA
Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA
Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TP Mazembe katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliopigwa uwanja wa TP Mazembe huko Lubumbashi, DR Congo
Bao la Farid Mussa lililopatikana kwenye kipindi cha pili lilitosha kuihakikishia Yanga ushindi huo muhimu ambao unaweza kuwahakikishia kumaliza vinara wa kundi D
Krosi ya Jesus Moloko ilimshinda mlinda lango wa Mazembe kabla ya kuangukia mguuni kwa Farid aliyeujaza mpira kimiani kwa mguu wake wa kulia
Ilikuwa mechi ngumu iliyopigwa katika uwanja wa nyasi bandia ambao kwa kiasi kikubwa uliwapa wakati mgumu wachezaji wa Yanga huku wenyeji wakitawala
Yanga imefikisha alama 13 wakati US Monastir wana alama 10 wakitarajiwa kucheza na Real Bamako saa 4 usiku
Ili kuishusha Yanga kileleni, Monastir watahitaji kushinda kuanzia mabao matatu
Post a Comment