Matokeo Simba vs Wydad Athletic Leo April 22,2023

Ofa ya Bando la Internet wiki BURE Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Bingwa mtetezi amepigika mbele ya Simba! Ndio ushindi wa bao 1-0 umeiweka Simba kifua mbele kuelekea mchezo wa marudiano robo fainali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Wydad Athletic


Jean Baleke ameendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akifunga bao lake la nne katika michuano hiyo leo


Kazi nzuri kutoka kwa Kibu Denis kwenye dakika ya 41 ilimaliziwa vyema na Baleke aliyewazidi ujanja walinzi wa Wydad


Kipindi cha kwanza Simba ilicheza kwa tahadhari kubwa lakini kipindi cha pili iliongeza kasi na pengine ilistahili kufunga mabao zaidi Kibu Denis, Chama wakikosa nafasi


Ushindi wa nyumbani ni muhimu, vijana wa Robertinho Oliveira wanahitaji kwenda Morocco kwenda kulinda ushindi huo ili kukata tiketi ya kutinga nusu fainali

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post