Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Simba ilihitaji dakika 45 tu kumaliza mchezo wakipachika mabao manne huku mshambuliaji Jean Baleke akiendeleza kasi yake ya kuzifumania nyavu akiondoka na mpira baada ya kufunga hat-trik
Baleke sasa amefunga mabao 12 katika mechi tano zilizopita akiwa na wastani wa kufunga zaidi ya mabao mawili katika kila mchezo
Saido Ntibazonkiza naye akaingia kambani akiweka bao la nne huku Pape Ousmane Sakho akiweka bao la tano kwenye dakika za majeruhi
Ihefu Fc walifunga bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Raphael Daudi
Katika kipindi cha pili kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira alifanya mabadiliko kwa kuwatoa baadhi ya nyota wake muhimu huku akiwapa nafasi Jonas Mkude, Mohammed Mussa Kennedy Juma na Beno Kakolanya walioingia kuchukua nafasi za Hennock Inonga na Aishi Manula walioumia
Simba sasa imetinga nusu fainali ya michuano hiyo ambapo itachuana na Azam Fc katika mchezo utakaopigwa Nangwanda Sijaona, mkoani Mtwara
Post a Comment