Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Safu ya ulinzi ya Manchester United imeendelea kuonyesha udhaifu mkubwa katika jitihada zao za kujijenga upya kufuatia makosa mengi katika mchezo wa mkondo wa pili robo fainali ya ligi ya Europa dhidi ya Sevilla
Man United ilitolewa kwenye mashindano hayo Jana usiku baada ya Sevilla kuwacharaza 3-0 na kuwaondosha kwa jumla ya mabao 5-2
Baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 kabla ya mabao mawili ya kujifunga wenyewe mwishoni mwa mechi ya kwanza, Man United walikuwa na matumaini kwamba wangeweza kufika nusu fainali nyingine baada ya kushinda Kombe la Carabao na kutinga nusu fainali ya Kombe la FA
Lakini haikuwa hivyo, kwani makosa yao yaliwagharimu huku Youssef En-Nesyri na mchezaji wa zamani wa Nottingham Forest Loic Bade wakifunga mabao yaliyoipeleka Sevilla nusu fainali.
Baada ya kipigo hicho, mkufunzi wa Manchester United Erik ten Hag amekiri kuwa ipo changamoto katika safu yake ya ulinzi na kwa sasa ni lazima wakubali ili kupata ufumbuzi wa changamoto hiyo
Post a Comment