Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabao ya Karim Benzema na Marco Asensio yaliihakikishia Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya uliopigwa Jumatano usiku
Ushindi huo umeiweka Real Madrid katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali kwani watahitaji matokeo ya sare hata kufungwa sio zaidi ya bao moja
Pamoja na kipigo hicho, mkufunzi wa muda wa Chelsea Frank Lampard amesema wachezaji wake wataendelea kuwa na imani kuwa wanaweza kufanya kitu nyumbani
AC Milan ilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Napoli katika mchezo mwingine wa robo fainali uliohusisha derby ya Italia
Timu hizo zitarudiana tena wiki ijayo kwenye uwanja wa Diego Maradona huko Napoli
Post a Comment