Matokeo Raja Casablanca vs Simba haya hapa

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Usiku wa kuamkia leo Simba ilikamilisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakikubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Raja Casablanca katika mchezo uliopigwa uwanja wa Mohammed V nchini Morocco


Katika kipindi cha kwanza Simba ilionekana kucheza kwa nidhamu kubwa wakiwanyima Raja nafasi ya kuipenya kirahisi ngome yao


Hata hivyo wakati mchezo ukielekea mapumziko, safu ya ulinzi ya Simba ilipoteza umakini wake ikawa rahisi kwa Khabba kuiandikia Raja bao la kuongoza kwenye dakika ya 44 baada ya kumzidi ujanja mlinzi wa Simba Joash Onyango


Kwenye kipindi cha pili Simba walirejea tofauti na iliwachukua dakika tatu tu kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jean Baleke ambaye aliweka mpira katia nyavu tupu baada ya makosa ya mlinda lango wa Raja aliyekuwa ametoka langoni


Kuingia kwa bao hilo ni kama kuliwaamsha Raja na kupeleka mashambulizi mfululizo katika lango la Simba


Dakika ya Joash Onyango tena akamfanyia madhambi Khabba ndani ya eneo la hatari na mwamuzi kuamuru pigo la penati


Khabba hakufanya ajizi akaifungia Raja bao la pili. Boulacsoul akaongeza la tatu kwenye dakika ya 86


Simba sasa inasubiri droo ya hatua ya robo fainali itakayopigwa April 05 huko Misri

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post