Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Manchester City ilipiga hatua kubwa kuelekea nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Bayern Munich katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa robo fainali uliopigwa Etihad Jumanne usiku
Rodri, Bernardo Silva na Erling Haaland walifunga mabao kwa mabingwa hao wa Premier League wakiwa katika kiwango bora kabisa
Iliwachukua Manchester City karibu nusu saa kuandika bao la kwanza, lakini umaliziaji wa kiwango cha kimataifa kutoka kwa Rodri kutoka nje ya eneo la hatari uliwapa Waingereza bao la kuongoza
Kulikuwa na dalili za uwezekano wa kurejea mchezoni kwa wageni mwanzoni mwa kipindi cha pili lakini City waliongeza bao la pili ndani ya dakika sita huku Haaland akitoa pasi nzuri ya bao la Silva kabla ya kuifungia City bao la tatu
Kikosi cha Pep Guardiola kitasafiri hadi Allianz Arena kikiwa na faida ya mabao matatu kwa moja kwenye mkondo wa pili Jumatano ijayo.
Post a Comment