Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Sio mwingine! Ni yuleyule Jean Baleke magoliiiii, amewalaza na viatu Ihefu Fc huko Mbarali, Mbeya
Mabao yake ya dakika za jioni yemetosha kuihakikishia Simba ushindi wa mabao 2-0 na kuzoa alama zote tatu
Kikosi cha Simba leo kimewapa somo mashabiki wake, ni muhimu kuwa na imani na timu yao
Lawama zilikuwa nyingi baada ya kocha Robertinho Oliveira kufanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake akiwaacha nje nyota wake muhimu
Leo Robertinho ni mshindi na wale waliokuwa wakiponda uamuzi wake wanapaswa kutumia nguvu ileile kumpongeza
Baleke amewafunga Ihefu Fc mabao matano katika kipindi cha siku tatu
Huyu ni mwamba kwelikweli! Hawa Mbogo Maji hawatamsahau kamwe..!
Ni ushindi muhimu kwa Simba ambao unaongeza presha katika mbio za ubingwa sasa zikibaki alama tano tu
Post a Comment