Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabingwa watetezi Ligi Kuu ya NBC, Yanga leo wako uwanjani kuikabili Kagera Sugar katika mchezo wa ligi hiyo raundi ya 25
Mchezo huo wa kiporo utapigwa saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Wakati Ligi ikielekea ukingoni, Yanga inasaka alama tisa kutoka kwenye mechi sita zilizosalia ili kujihakikishia ubingwa wa 29
Ushindi dhidi ya Kagera Sugar utawafanya wazidi kukaribia taji la pili mfululizo
Ni wazi mchezo huo hautakuwa mwepesi kutokana na ubora wa Kagera Sugar hasa wanapokutana na Yanga
Jana katika Mkutano na Wanahabari, Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alikiri Kagera Sugar waliwapa wakati mgumu kwenye mchezo wa duru ya kwanza uliopigwa uwanja wa CCM Kirumba ingawa walishinda bao 1-0
Kaze alisema leo wanahitaji kuwa katika ubora wao ili kuweza kushinda mchezo huo
Habari njema kwa Yanga ni kuwa kwa sasa hawana changamoto kubwa ya wachezaji majeruhi, Aboutwalib Mshery ndiye mchezaji pekee anayekosekana
Yanga inahitaji kushinda ili kurejesha gap la alama nane dhidi ya watani zao Simba ambao jana walipata ushindi dhidi ya Ihefu Fc na kufikisha alama 60
Matokeo tofauti na ushindi ni wazi yatawaongezea presha kuelekea dabi ya Kariakoo itakayopigwa Jumapili, April 16 2023 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Post a Comment