Matchday Live : Yanga vs Geita Gold

Kuingiza pesa Mtandaoni bure Bonyeza HAPA


Ajira Mpya zilizotangazwa leo Bonyeza HAPA


Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA


 Mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga leo majira ya saa 2 usiku watashuka uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es salaam kumenyana na Geita Gold katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)


Wakiwa mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Yanga inahitaji kushinda mchezo huo ili kukata tiketi ya kutinga nusu fainali


Hata hivyo wanakutana na Geita Gold ambayo mara kadhaa imekuwa sio timu rahisi pale ilipokutana na Yanga


Mara ya mwisho Yanga na Geita Gold zilikutana hapohapo kwenye uwanja wa Azam Complex kwenye mchezo wa ligi kuu Wananchi wakiibuka na ushindi wa mabao 3-1


Geita Gold waliweka kambi ya takribani wiki moja jijini Dar es salaam kujiandaa na mchezo huo huku Afisa wao wa habari Hemed Kivuyo akitamba kuwa leo watalipa kisasi


Kocha Msaidizi wa Yanga Cedric Kaze alisema wachezaji wote wako tayari kwa mchezo huo, mlinda lango Aboutwalib Mshery ndiye mchezaji pekee ambaye atakosekana akiwa ni majeruhi


Mshindi wa mchezo huo ataungana na Singida BS, Azam Fc na Simba ambazo tayari zimetangulia nusu fainali

Mechi Itakuwa LIVE kwenye App yetu ipakue Sasa bofya hapa kuidownload ili usipitwe na mechi hii LIVE kupitia simu Yako

0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post