Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Kikosi cha Simba kiko mkoani Mbeya ambapo jioni ya leo kitakuwa uwanjani huko Mbarali kumenyana na Ihefu Fc katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Ihefu katika mchezo wa robo fainali kombe la FA uliopigwa uwanja wa Azam Complex, April 07 Simba ikitinga nusu fainali
Hata hivyo mchezo wa leo unatarajiwa kuwa tofauti ambapo Kocha Mkuu wa Simba Robertinho Oliveira amesema kikosi chake kitahitaji kudhihrisha ubora kwa mara nyingine kwa kushinda mchezo huo
Simba inahitaji kushinda mchezo huu ili kuendelea kuweka hai matumaini katika mbio za ubingwa msimu huu
Simba inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa nyuma kwa alama nane dhidi ya Yanga
Katika mechi sita zilizosalia kuhitimisha msimu, mkakati wa Simba na kuvuna alama tatu katika kila mchezo
Post a Comment