Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Mabingwa wa Ligi Kuu ya NBC Yanga ambao ni vinara wa kundi D, leo wako ugenini huko Lubumbashi DR Congo kuikabili TP Mazembe
Mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 10 jioni kwa saa za Tanzania (saa 9 DR Congo), utakuwa wa kukamilisha ratiba tu kwa TP Mazembe kwani matokeo yoyote hayana athari kwao
Lakini kwa upande wa Yanga, ushindi unaweza kuwahakikishia Wananchi kumaliza makundi wakiwa vinara wa kundi D. Yanga tayari imefuzu hatua ya robo fainali
Yanga ilipata siku mbili za kujiandaa huko Lubumbashi ikikamilisha mazoezi ya mwisho katika uwanja wa TP Mazembe jana jioni
Kikosi cha Yanga leo kitaongozwa na Kocha Msaidizi Cedric Kaze baada ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi kushindwa kusafiri kutokana na matatizo ya kifamilia
Kaze amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa timu yao iko kamili kuwania ushindi katika mchezo huo unaoarajiwa kuwa na upinzani mkali
Mechi Itakuwa LIVE kwenye App yetu bofya hapa kuidownload mapema ili usipitwe na mechi hii
Post a Comment