Msimamo wa ligi kuu Tanzania Bonyaza HAPA
Manchester City imeweka hai matumaini katika mbio za kuwania ubingwa wa Premia baada ya kuichapa Liverpool mabao 4-1 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Etihad
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola alijua ni lazima ashinde mechi hiyo City waliingia dimbani wakiwa nyuma kwa tofauti ya alama nane dhidi ya vinara wa ligi Arsenal
Liverpool walitangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Mohamed Salah wakati Diogo Jota alipovunja mtego wa kuotea kabla ya kumtengenezea Salah kuuweka mpira kimiani.
City walirudi na moto na haikuchukua muda kabla ya kupata bao la kusawazisha kupitia kwa Julian Alvarez baada ya pasi murua kutoka kwa Jack Grealish
Mabao mengine ya Manchester City yalifungwa na Kevin de Bruyne, Grealish na Ilkay Gundogan wakihakikisha wanarejea kwenye mbio za ubingwa sasa wakitofautiana na Arsenal alama tano kabla ya mechi ambayo Arsenal wanakabiliana na Leeds United
Ni moja ya siku mbaya kwa Liverpool katika ligi kuu ya Premia msimu huu kwani ukiondoa bao walilofunga, hawakuwa na hatari yoyote kwenye lango la Man City
Post a Comment