Yanga iko Nigeria ambapo jioni ya leo majira ya saa 10 kwa saa za Tanzania, itashuka uwanja wa Godswill Akpabio International kuwakabili wenyeji wao Rivers United katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ya kombe la Shirikisho la CAF barani Afrika
Msimu huu umekuwa wa mafanikio makubwa kwa Yanga katika michuano hiyo, matumaini ya Wananchi ni kuona timu yao inaendelea kun'gara katika michuano hiyo
Kikosi cha kocna Nasreddine Nabi leo kina kazi moja tu, kusaka ushindi au matokeo ya sare ugenini ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali katika michuano hiyo
Ikumbukwe dakika nyingine 90 za mkondo wa pili zitapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili ijayo, April 30
Katika Mkutano na Wanahabari jana, Nabi alisema wanatambua ubora wa Rivers United, wamejipanga kukabiliana nao
Nabi alisema timu yake inamabadiliko makubwa ukilinganisha na kikosi alichokuwa nacho mwanzoni mwa msimu uliopita ambacho kilipoteza mechi zote mbili hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Rivers United
Leo utakuwa mchezo tofauti na dhamira ya Yanga ni kupata matokeo mazuri yatakayowaweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali pale tmu hizo zitakaporudiana nchini Tanzania wiki ijayo
Mchezo utapigwa majira ya saa nane mchana kwa saa za Nigeria (saa 10 Tanzania Pia mechi Itakuwa LIVE kwenye App yetu bofya hapa kuidownload mapema kutoka Play store ili uweze kuitazama mechi hii buree
Post a Comment